Huduma za afya kuimarishwa katika Hospitali ya Elburgon


Waziri wa Afya katika kaunti ya Nakuru Roselyn Mungai amesema kuwa serikali ya kaunti imeweka mipangilio kabambe kuhakikisha kuwa huduma za afya katika hospitali ya Elburgon zinaimarishwa.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika hospitali hii alipofanya mkutano pamoja na bodi ya usimamizi, Mungai alisema kuwa mipango hii inayonuia kuanza kutekelezwa baada ya mwezi mmoja italeta ongezeko la wateja wanaohudumiwa mjini Elburgon na hata maeneo jirani kwa mara mbili zaidi.

Ili kufanikisha juhudi hii, waziri alisema kuwa tayari ununuzi wa vifaa muhimu vya matibabu unaendelea na vitawezesha pia kuboresha miundombinu muhimu hospitalini kama vile katika chumba cha kujifungulia cha akina mama, chumba cha upasuaji, picha baadhi ya maeneo mengine pia.

Aidha, Mungai alisalia na imani kuwa ikiwa hatua hizi zitatekelezwa, basi bila shaka changamoto nyingi zitaweza kushughulikiwa akiwaomba wafanyikazi mahala pale kuendelea kuyasikiliza matakwa ya wakaazi katika utoaji huduma bora ya afya ili wawe katika mstari wa mbele k
uwahudumia vilivyo.

Kwa muda, hospitali hii imekuwa na uwezo wa kushughulikia wagonjwa 3,000 kwa siku.

Source: Kenya News Agency